Mke wa Kingunge afariki...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras amefariki  leo  alhamisi majira ya saa nane mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH). Kifo hicho kinatokea huku Kingunge akiwa mgonjwa kutokana na kung'atwa na mbwa hivi karibuni















Mke wa Kingunge, Peras























Mke wa Kingunge,Peras






Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha kifo hicho na kwamba taratibu za mazishi zinaendelea na ratiba itatolewa


Afisa uhusiano Muhimbili, John Steven ameiambia matukio360 kuwa mke huyo wa Kingunge alifika Muhimbili Oktoba 3, 2017 akitokea hospitali ya Kairuki na pia Kingunge anapatiwa matibabu Muhimbili.

" Siwezi kusema alikuwa anaumwa nini, alikuwa akipatiwa matibabu tangu Oktoba 3, 2017 akitokea hospitali ya Kairuki. Amefariki majira ya saa nane mchana leo alhamisi Disemba 4, 2018," amesema Steven

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search