TLP: CCM, Chadema hawafai ubunge Kinondon,Siha...soma habari kamili na matukio360....#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


CHAMA cha Tanzania Labour Party (TLP) kimesema wagombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Mapinduzi (CCM) Siha na Kinondoni hawafai.

Mgombea Ubunge wa Chama cha TLP, Jimbo la Kinondoni Dk. Godfrey Malisa (watatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi katika Jimbo hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na mgombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama hicho(Kinondoni), Dk. Godfrey Malisa kutokana na kukerwa baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo Kinondoni kupitia Ukawa, Maulid Mtulya kuhamia CCM.


Amesema wananchi wawe makini na mgawanyiko unaoendelea na kwamba wamchague kwakuwa hakuna Ukawa kwenye uchaguzi mdogo wa marudio hivyo watagawanya kura na kuwapa ushindi CCM.


"Tutafika mahali tutashindwa kupata kura za kutosha kuwazuia CCM wasiingie madarakani,  chadema walisimama wakatuletea mtu wakati ule wa Ukawa... Mtu huyo tunajua alichokifanya, "amesema.


Ameongeza kuwa "Chadema hao wakasimama wakatangazia umma wa Watanzania kwamba hawataki kushiriki chaguzi zinazofuata kwasababu wanaona wananyanyaswa na kudhulumiwa wakagomea uchaguzi wa Songea, Singida na Loliondo wakisema hakuna haki, "amesema.


Dk. Malisa amehoji kuwa Chadema wameona nini kwenye uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni haliyakuwa awali walitangaza kutoshiriki uchaguzi? Huku mazingira yakiwa ni yale yale!


"Kuna hatari ya kugawanyika kama kusipokuwa na msimamo wa wapiga kura wa Kinondoni...kama kweli unauchungu Jimbo hili lisirudi CCM nipe kura yako, "amesema.


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Richard Lyimo amesema TLP hawana ugomvi na Ukawa na kwamba  vyama vingine vilishindwa kuweka wagombea wakitegemea Ukawa hautashiriki.


"Chadema alivyofanya maamuzi ya kushiriki uchaguzi hakuna kikao wala maamuzi yaliyoshirikisha vyama vilivyokuwa Ukawa, hivyo Chadema waliamua tu kuvunja demokrasia ndani yao kwa sababu ya maamuzi yao ya mwisho mwisho ambayo yaliwalazimisha kushiriki uchaguzi, "amesema.


Amefafanua kuwa"Kama Chadema wangeshikilia msimamo wao wa kutokushiriki, sisi tungeshiriki.... Ndiyo tulivyokuwa tumeweka sisi, mgombea wetu tumemuandaa siku nyingi tukijua kwamba Chadema haishiriki kama ilivyosema na tuliamini hakuna kikao kilichokaa kujadili matatizo ambayo wao waliamini hayatawasaidia kwenye uchaguzi".


Amesema  chama hicho kimeweka mgombea kwakuwa hakukuwa na Ukawa wala Chadema inayoshiriki lakini baadae wakageuza ndege angani kwa kuweka mgombea.


Amesema chadema imeonesha kutokuthamini wagombea wa vyama vingine na kujivunjia heshima kwa viongozi wao kwa kuwadanganya wananchi na kuonesha kutokuwa na mahusiano mazuri na wapiga kura wao.


"Kurudi kwao kunatuathiri sisi kwasababu watanzania hawatatuamini sisi wapinzani,watatuathiri kwa wapiga kura sisi wapinzani hatuaminiki tunaongea uongo ndiyo athari yetu sisi, "amesema.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search