TRA kusajili walipa kodi milioni 1...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Salha Mohamed, Dar es salaam
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mwaka 2018 inatarajia kusajili walipa kodi milioni moja na sasa inawalipa kodi milioni 2.5 katika daftari la walipa kodi nchini ambapo 475 ni walipa kodi wakubwa.
Kamishna wa Kodi za ndani, Elijah Mwandumbya (wa tatu kushoto) akizungumzia uzinduzi wa kampeni ya usajili wa walipa kodi nchini inayoanza leo,(wa kwanza kushoto) Meneja Elimu kwa mlipa kodi, Diana Masalla,Mkuregenzi wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo na Mkurugenzi Msaidizi Habari Maelezo, Rodney Thadeus.
Kamishna wa Kodi za ndani wa Mamlaka hiyo,Elijah Mwandumbya ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usajili wa mlipa kodi nchini.
"Katika kampeni hii mwaka wa fedha 2018 tumepanga kusajili walipa kodi milioni moja na tunakwenda vizuri mikoa yote,"amesema.
Amefafanua kuwa kwa mwaka huo wa fedha wanatarajia kukusanya sh bilioni 44 ikiwa ni kodi ya majengo nchini.
Amesema katika michezo ya kubahatisha, mamlaka hiyo inatarajia kukusanya kodi sh bilioni 25.
Akizungumzia kampeni hiyo, Mwandumbya amesisitiza kuwa usajili wa TIN ni bure hivyo wananchi hawapaswi kulipa kwa yeyote.
"Kwa walipa kodi wadogo wanaostahili kulipa kodi kwa makadirio badala ya kutayarisha mahesabu, robo ya ya kwanza ya malipo watailipa ndani ya siku 90 kuanzia waliposajiliwa,"amesema
Amesema utaratibu huo ni tofauti na utaratibu uliokuwepo awali wa kulipia kodi hata kabla hajaanza kufanya biashara.
Amesema mamlaka hiyo haijaweka wakala aliyepewa jukumu la kusajili au kutoa fomu za usajili hivyo wananchi wajihadhari na vishoka wenye nia ya kuharibu kampeni.
"Naomba wafanyabiashara wote waliokuwa na biashara bila kuwa na TIN au kama walikwamishwa siku za nyuma wajitokeze ili waweze kusajiliwa na kupatiwa bila malipo, "amesema.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.




No comments:
Post a Comment