Walemavu 143 wapewa miguu bandia...soma habari kamili na matukio 360..#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


JUMLA ya walemavu 143 wamepata miguu ya kisasa ya bandia yenye thamani ya sh. milioni 481 bure.

Baadhi watu wenye ulemavu waliopewa miguu bandia wakitembea nayo.

Walemavu hao wamepata miguu hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ya kuwapatia miguu ya kisasa itakayowawezesha kufanya shughuli zao za uzalishaji mali kama awali.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, inaeleza kuwa hiyo ni  awamu ya pili, awamu ya Kwanza walemavu 108 walipewa miguu ya kisasa ya bandia yenye thamani ya shilingi milioni 324 na  kuwa mguu mmoja unagharimu shilingi milion 2 hadi 3.


Taarifa hiyo inaeleza  jumla ya wagonjwa 35 wa kisukari walipata miguu ya kisasa ya bandia yenye thamani ya shilingi milioni 157 kutoka hospitali us CCBRT.

Baadhi ya Walemavu waliopatiwa miguu hiyo wamemshukuru Makonda na kwamba wataenda kufanya kazi na kuachana na utegemezi.


Aidha wameishukuru kampuni ya Kamal Group kwa kumuunga mkono Makonda kutimiza maono yake ya kuwawezesha walemavu kupata miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za kujiingizia kipato.

Baadhi  ya watu wenye ulemavu waliopewa miguu bandia, wakiiweka mguuni tayari kwa kuitumia

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search