Zimamoto Geita waokoa mamilioni ya fedha..soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Geita

ASKARI wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita wameokoa fedha takribani milioni nane pamoja na vitu mbalimbali katika zoezi la kuzima moto uliokuwa ukiteketeza nyumba
Mamilioni ya fedha yaliyokuwa yakiteketea kwa moto mkoani Geita eneo la Katoro, yakiokolewa.


Nyumba hiyo inayomilikiwa na  Magdalena Bujashi( 46) iliyopo eneo la Katoro Mkoani Geita iliripotiwa kushika moto na taarifa za moto huo kufika ofisi za Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Geita saa mbili na dk 20 asubuhi ya jana  Januari 19, 2018 kwa njia ya Simu.

Kikosi hicho kilifanikiwa kuudhibiti moto moto pamoja na kuokoa kiasi hicho cha pesa na hakukuwa na madhara kwa binadamu.
Askari wa zimamoto wakizima moto

Vitu vilivyoteketea kwa moto

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search