Watumishi 28 serikalini wafukuzwa kazi....soma habari kamili na matukio 360...#share
Na Mwajuma Kombo, Zanzibar
WATUMISHI 28 kutoka Wizara ya Elimu Zanzibar wamefukuzwa kazi kutokana na makosa mbali mbali ikiwemo ubadhirifu wa fedha wa zaidi ya shillingi millioni mia moja.
Katibu mkuu kiongozi Zanzibar, Abdul Hamid Yahya Mzee
Hayo uamebainishwa na Katibu Mkuu Kiongozi wa Baraza la Mapinduzi
Zanzibar Abdul-Hamid Yahya Mzee wakati alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake Ikulu.
Alisema kuwa walimu hao ambao majina na shule wanazosomesha
yamehifadhiwa mbali ya kupewa adhabu hiyo pia watalazimika kulipa
fedha hizo, ambapo tayari milioni 82 na laki mbili zimesharejeshwa.
Uwamuzi wa Serikali wa kuchukuwa hatua hiyo umetokana na Uhakiki
uliofanywa katika utendaji wa majukumu yao na kubainika kuwa
wanafanya kazi kunyume na utaratibu wa kisheria.
Amefahamisha kwamba walimu hao walibainika kufanya makosa matatu tofauti ambayo miongoni mwao wakiwa baadhi yao wameshastaafu na wengine hawahudhuri kazini huki wakiendelea kupokea mishahara kinyume na utaratibu .
Amesema kati ya walimu nane ni wagonjwa wa muda mrefu kati yao
watano wanaendelea na uchunguzi wa kiafya ,wawili waligundulika kuwa wazima na mmoja ameshastaafishwa kutokana na ugonjwa.
Amesema kuna walimu wengine pia walikuwa wameshastaafu
lakini walikuwa wakiendelea kupokea mishahara wengine kuchukua likizo bila malipo.
Kufatia hatua hiyo Serikali imeiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali kuendelea kuwatafuta walimu ambao hawajapatikana ili waweze
kuchukuliwa hatua za kisheria pamoja na kurejesha fedhaa za mishahara walizoingiziwa.
Akizungumzia Wizara ya Afya amesema kumejitokeza kosa moja la upotevu wa mshahara wa mfanyakazi wa kigeni ambaye hayupo nchini
lakini mshahara wake unapokelewa na mtu asiejulikana. Amesema tayari hatua za kiuchunguzi zinaendelea ili kumbaini

No comments:
Post a Comment