Waziri mkuu aagiza milioni 320 zilizoibwa zirejeshwe ....soma habari kamili na matukio 360...#share
Na Mwandishi wetu, Mara
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Ofisa
Ushirika wa Manispaa ya Musoma, Yunia Wiga kufuatilia upotevu wa sh. milioni 320
za Imara SACCOS na atakayebainika kuhusika ashughulikiwe.
Waziri Mkuu Kassim Maja
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Waziri Mkuu, alitoa kauli hiyo jana jioni
alipopokea malalamiko ya wanachama wa SACCOS hiyo kupitia mabango
waliyoyawasilisha katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
Mukendo mjini Musoma.
Katika hatua
nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma Bibi Fidelica
Myovella kuhakikisha anatenga fedha kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi
mbalimbali waliopisha miradi ya maendeo katika Manispaa hiyo.
Waziri Mkuu alisema
siyo vizuri kwa halmashauri kuchukua maeneo ya wananchi kwa ajili ya ujenzi wa
miradi ya maendeleo kama barabara, standi na kisha kukaa muda mrefu bila ya
kuwalipa fidia zao.
Aliyasema hayo
baada ya kupokea malalamiko ya wananchi waliopisha ujenzi wa kituo cha daladala
cha Bweri ambao hawajalipwa fidia zao tangu mwaka 2013. Mkurugenzi huyo aliahidi
kuanza kulipa madeni hayo kuanzia mwezi Januari, 2018.
Awali, Mbunge wa jimbo la Musoma Mjini, Vedastus Mathayo aliishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza baadhi ya ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ikiwemo ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Mathayo alisema wananchi wa jimbo hilo kwa muda mrefu walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, hivyo alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa utekelezaji wa ahadi hiyo.
Mbali na mradi wa maji pia Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo ikiwemo ya ujenzi wa barabara za mitaa kwa kiwango cha lami pamoja na ukarabati wa kiwanja cha ndege unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Waziri Mkuu alisema ahadi zote zilizopo kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 na zile zilizotolewa na Rais Dkt. Magufuli zitatekelezwa, hivyo wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao.
No comments:
Post a Comment