Waziri Jafo ateta na wakuu wa wilaya, wakurugenzi...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuheshimu mipaka yao ya kazi, kuboresha mahusiano kazini, kutunza Siri za Serikali na kusimamia Maadili katika maeneo ya kazi.
Pia ameagiza maeneo ambayo bado kuna wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama yalioezekwa Nyasi au kujengwa kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja kutumia madarsa hayo na kujenga madarasa bora.
Pia ameagiza maeneo ambayo bado kuna wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama yalioezekwa Nyasi au kujengwa kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja kutumia madarsa hayo na kujenga madarasa bora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhe.Selemani Jafo akifungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakugenzi wa Halmashauri yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ushirikiano wa Taasisi ya Uongozi yanayofanyika kwa siku Tano Mjini Dodoma.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati
akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi
yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Taasisi ya
Uongozi yenye lengo la kujenga uwezo wa viongozi kuweza kutawala kwa ufanisi.
“Viongozi wangu nataka Mkakusanye mapato
ya ndani kwa nguvu zote na Fedha hizo mzitumie kwenye miradi ya maendeleo na
kwa wale ambao mpaka leo wanafunzi wanasomea kwenye mazingira duni hawana
madarasa bora watoto wanasomea kwenye madarsa ya Tembe, mengine yameezekwa kwa
Nyasi nahitaji muelekeze Nguvu katika ujenzi wa madarasa bora na hayo ya Tembe
yotoweke kabisa; Mjenge madarasa ambayo wanafunzi watajiskia fahari
kusoma”Alisema Waziri Jafo.
Waziri Jafo hakusita kuwakumbusha
Viongozi kuhusu Usimamizi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Afya 212
vinavyoendelea kujengwa hivi sasa katika ameneo yote yote Nchini.
Niwapongeze baadhi ya Wakurugenzi ambao
mpaka sasa wamefanya kazi nzuri sana ya Usimamizi wa ujenzi wa Miundombinu hiyo
ya Afya wameshakamilisha ujenzi na wamejenga mpaka Njia za kutembelea(Walk Way)
katika vituo hivyo na nataka mpaka Tarehe 30 April 2018 Kila Halmashauri
iliyopokea Fedha za ujenzi wa Miundombinu ya Afya iwe imekamilika.
Awali akizungumza katika Ufunguzi wa
Mafunzo ya Uongozi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph
Semboja amesema kuwa mafunzo haya yanakamilisha mtiririko wa mafunzo
yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Majaliwa K. Majaliwa miezi nane iliyopita na baada ya mafunzo haya yanayoanza
leo tutakuwa tumewafikia Viongozi 324.
Prof.Semboja aliongeza kuwa Lengo la
mafunzo haya ni yale yale ambayo ambayo yamelengwa tangu Kikao cha Mwanzo cha
Mafunzo haya ambayo ni kuimarisha uwezo wa kufanya maamuzi wa Kimkakati
kwa kuzingatia mahitaji ya jamii kwa manufaa mapana ya sasa nay a baade
ya Jamii Tunayoihudumia.
Sambamba na hilo Mkutano huu pia
unalenga kuongeza uwezo wa Viongozi wetu katika kuongoza watu na rasillimali
zingine zilizoko kwenye maeneo yetu ili kwa pamoja tuweze kufikia malengo ya
pamoja.
Alisisitiza kuwa Mafunzo haya
yatajielekeza katika Kuimarisha Sifa Binafsi za Viongozi kwa sababu
Viongozi ndio wanaowasimamia wananchi katika kiLA Eneo hivyo ni lazima kila
kiongozi aweze kujitenegenezea Sifa binafsi ili akubalike na kuhesimika katika
Jamii husika.
“Sifa hizi binafsi tunazozizungumzia ni
Ushawishi, Kuaminika, Uadilifu, Mtenda Haki, Muumini wa Utawala bora na Utawala
wa Sheria na zaidi kuwa mchahapa kazi na awe na weledi wa hali ya juu sasa haya
yote yatafundishwa kupitia mafunzo haya ya namna gani Kiongozi anaweza
Kujijengea Sifa Binafsi katika Jamii tunazoziongoza.
Akitoa Neno la Shukrani kwa niaba ya
viongozi walioshiriki katika Mafunzo haya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph
Mkirikiti ameshukuru OR-TAMISEMI na Taasisi ya Uongozi kwa kuandaa mafunzo haya
na zaidi ameahidi Umakini wa washiriki kwa siku zote za mafunzo.
Mafunzo haya ya awamu ya Nne na ya
mwisho kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa
imegususa Viongozi kutoka katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga,
Kilimanjaro na Arusha.
No comments:
Post a Comment