Yajue magonjwa yanayowasumbua wakazi Dar es salaam...soma habari kamili na matukio 360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
MGANGA Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Dk. Grace Maghembe amesema magonjwa sugu yanayoongoza kuwaathiri
wakazi wa jijini hapa ni kisukari, moyo na shinikozo la damu.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Grace Maghembe akikata utepe kwenye uzinduzi wa kituo cha afya Aga Khan Ukonga jijini hapa.
Dk. Maghembe amesema
hayo leo alipokuwa akizindua kituo cha
afya cha Aga Khan Ukonga jijini Dar es Salaam, amesema sababu ni tabia na mienendo ya wakazi kula vyakula vya wanga kwa wingi bila kufanya
mazoezi.
“Takwimu za magonjwa
yanayoongoza ni kisukari, moyo na shinikizo la damu, hutokana na mfumo wa
maisha, tunakula vyakula vya wanga kwa wingi bila mazoezi hivyo vinabadilika kuwa mafuta,”
amesema Dk. Maghembe.
Pia amesema kwa watoto
wadogo wanaathiriwa zaidi na ugonjwa wa kifua.
Akizungumzia kituo cha
afya kilichozinduliwa, amewapongeza Aga Khan kwa kusogeza huduma za afya nje ya
mji na kuwaomba wapunguze gharama kwa wakazi wa eneo hilo ili waweze kupata
huduma kwa gharama nafuu.
Amesema serikali
itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji katika sekta ya afya ili
kufanikisha lengo la kuporesha huduma kwa wananchi kwani serikali serikali peke
yake haiwezi kukidhi mahitaji.
Ameomba kituo hicho
kusaidia katika kuhudumia wananchi wenye bima ya afya na ametoa wito kwa
wananchi kujiunga na bima ya afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu wakati wowote
wanapohitaji.
Mkurugenzi Uendeshaji
wa Vituo vya Afya Aga Khan Tanzania Fayyaz Taqi amesema kituo hicho kimegharimu
sh.milioni 350 zilizotumika kwenye ukarabati wa jingo pamoja na vifaa tiba na
maabara.
Amesema kuwa kitakuwa
kikihudumia wagonjwa 100 hadi 150 kwa siku na kinakuwa kituo cha 9 kwa mkoa huu
ambapo malengo yao ni kujenga vituo 10.
Ameongeza kuwa
wameanzisha na kuendeleza mfumo wa afya jumuishi nchini ambao kwa pamoja na
upanuzi wa hospitali kuu ya Aga Khan unaogharimu sh. bilioni 176 na unelenga
kuongeza vitanda vya wagonjwa wa kulazwa, mafundisho na elimu ya tiba ya afya.
Ameeleza kwamba
wanafanya hayo samamba na kukuza mtandao wa vituo 35 vya uhamasishaji nchini
ambavyo vitachangia kuondokana na vikwazo visivyo muhimu vya upatikanaji wa
huduma bora za afya ili kufikia kuleta athari chanya juu ya hali ya afya ya
wananchi.
No comments:
Post a Comment