Zao la muhogo sasa dili China...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

WATANZANIA wamehimizwa kulima zao la muhogo kwa wingi kufuatia nchi ya  China kuhitaji bidhaa hiyo kwa wingi.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu waziri wa kilimo wa China Dk. Qu Yongyu na kwamba China itabadilishana tekinolojia ya kilimo, masoko na kujenga uwezo hususani katika matumizi ya nguvu kazi na wananchi wa Tanzania.


Waziri wa kilimo nchini Dk. Charles Tizeba na Naibu waziri wa kilimo wa China Dk. Qu Yongyu (wote katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa wizara hizo baada ya mazungumzo jijini Dar es Salaam.


Pia  Tanzania na China zimeunda kikosi kazi cha wataalam wa kilimo kitakachopitia makubaliano ya nchi hizo  kwenye masuala ya kilimo ili yaweze kutekelezwa kwa haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, waziri wa kilimo Dk. Charles Tizeba amesema moja ya makubaliano ni ushirikiano katika soko kwa wakulima kutokana na fursa kubwa katika soko la China ambalo linaweza kuwanufaisha watanzania kama fursa ikitumika vizuri.

“Huu ni mwendelezo wa mazungumzo yaliyofanywa na viongozi wakuu wa nchi hizi na katika mazungumzo yetu tumekubaliana kuanzisha kikosi kazi kitachopitia mambo tuliyokubaliana  ili yatekelezwa kwa haraka iwezekanavyo na tumeshapata viongozi watakaongoza kikosi hiki,” amesema Dk. Tizeba.

Amesema makubaliano mengine yatakayofanyiwa
kazi ni uhirikiano wa kitaaluma kati ya wanasayansi wakitanzania na wa china kubadilishana uzoefu na taaluma ya kilimo kwa ujumla.

"Na katika hili tumekubaliana kwamba Naibu waziri wa Kilimo Dk. Mwanjelwa katikati ya mwezi Mei, 2018 atakwenda China kuhudhuria maonesho ambayo yatakuwa yakihusisha  bidhaa mbali mbali za kilimo  ili kujifunza, na hii itasaidia kuleta mabadiliko katika sekta hii,” amesema.




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search