Mbeya mbioni kupata maji ya uhakika...soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu Mbeya. 


Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira,
Simeon Shauri amesema utekelezaji mradi mkubwa wa maji kutoka mto kiwira hadi Mbeya mjini na wilayani Mbalizi upo katika hatua za mwisho.

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, (katikati) akiwa na uongozi wa
Mamlaka ya maji safi na  usafi wa mazingira walipotembelea chanzo cha
maji cha mto kiwira Wilayani Rungwe ambacho kitatumi katika mradi
mkubwa utakaogharimu Bilioni 47 .

Ameleeza hayo katika ziara ya mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ya kukagua chanzo cha maji cha mto Kiwira wilayani Rungwe  na kukagua jengo la kisasa la mamlaka hiyo.


"Kulikuwa na changamoto kubwa sana ya  tatizo la maji katika baadhi ya
maeneo jijini hapa na mbeya vijijini sasa kupitia mradi huu tuna
uhakika  wananchi wataondokana na changamoto ya maji. Serikali imeshatoa bilioni 47 za mradi huu,"amesema.


Pamoja na mambo mengine Makalla ameagiza watumishi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya kufanya kazi kwa weledi na kujenga mahusiano mazuri na wateja pindi wanapotoa huduma.


Amesema utendaji kazi mzuri katika mamlaka hiyo ni kutoa
huduma bora katika jamii na kuepukana na vitendo vya rushwa.


"Ninawaagiza uongozi fuatilieni utendaji kazi wa watumishi, wengi
wanatoa huduma  hafifu lakini kwenye 'kuchart' wako vizuri sana sasa katika hilo ninakemea acheni mara moja na fanyeni kazi ya kuwahudumia wananchi.

Katika hatua nyingine ameiagiza mamlaka hiyo kufanya vipindi katika vituo
vya radio na televisheni ili kuelimisha jamii  kukabiliana na
uharibifu wa mazingira.

"Mbeya kuna radio nyingi mnashindwa kuzitumia sasa anzeni mfumo wa
kuvitumia kutoa elimu kwa jamii"alisema.
Meneja biashara wa Mamlaka hiyo , Venance Hawela amesema  mamlaka hiyo imekuwa ikikusanya mapato ya Sh milioni 800 kwa mwezi na kwamba
kuna wateja 52,000 kati ya hao 1,972 ni wa maji taka.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search