Alivyoagwa Kingunge Kongambale Mwiru....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abraham Ntambara, Dar es salaam

Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassani ameongoza mamia ya watanzania jijini Dar es Salaam  kuaga mwili wa mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru katika viwanja vya karimjee




Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa John Shibuda akitoa salamu za rambi rambi, amesema ameatuachia ufadhili wa maono ya kizalendo katika kupiga vita rushwa na ufisadi.

Amesema kutokwepo kwake tutakosa maono, busara na hekima zake hivyo watanzania na wadau wa siasa watakosa maono yake, kokosa historia na mwelekeo wa taifa.

Ameeleza kuwa mzee Kingunge ni shujaa wa kuishi katika imani zake za.kizalendo na hakuna mbadala wake.

Akitoa salamu za rambi rambi za Serikali Waziri Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa (Tamisemi) Suleman Jaffo amewataka watanzania na watumisha katika sehemu mbalimbali nchini kufuata mfano wa Mzee Kingunge Ngumbale Mwiri kuishi kiuzalendo.

Amesema kuwa serikali imapokea msiba huu kwa majonzo makubwa na kwamba ni wawatanzania wote kwani ni mmoja wa waasisi waliopigania taifa letu na kulipatia heshima kubwa.

Lakini pia amesema ni mmoja wa watanzania walioweza kuhudumu serikalini katika wazira ya Ofisi ya Rais, Seilikai za mitaa (Tamisemi?


Kingunge  aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita katika hospitali ya Taifa Muhimbili ( NMH) alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na mbwa wake nyumbani kwake jijini Dar es Salaam

Picha za matukio tofauti katika kuuaga mwili wa Kingunge leo





About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search