Mange Kimambi matatani, sheikh ampa siku 300...soma habari kamili na matukio360....#share.
Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
SHEIKH wa Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema mwaka huu utakuwa ni mwisho kwa mwanadada maarufu kwenye mitandao ya kijamii, Mange Kimambi kutukana viongozi wa Dini na Siasa.
Pia atauchukulia hatua za kisheria mtandao wa Jamii Forum, kwa kile walichodai Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), iangalie Sheikh Salum anafanya kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni unaotarajia kufanyika Febuari 17,2018.
Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam, Alhad Musa Salum akizungumza na waandishi was habari Leo jijini Dar es salaam
Sheikh Salum ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kusambaa kwa picha na taarifa kwenye mitandao ya kijamii(instagram) ikionesha Sheikh huyo akiwa amekaa pamoja na viongozi wa Chama cha Mapunduzi(CCM) na mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia na Kimabi kumtukana.
"...Mwaka huu ni mwaka wake wa mwisho, baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi wake au mkono wake, amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mikono yake ulimi wake ndiyo itamhalalishia kuangamia, "amesema.
Amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni na kuipigia debe CCM na kwamba picha ilipigwa wakiwa kwenye maziko ya Sheikh Masudi Ismail Kijitonyama Kinondoni, ambapo timu ya CCM iliingia na mgombea wao huku akiwa amekaa kwenye kiti na wakakaa karibu naye wakapiga picha zao.
Amefafanua kuwa yeye ni kiongozi wa dini na yupo kwenye kamati ya amani ya mkoa anaweza kualikwa na Chama chochote kwa kufanya sala na dua.
"Hata mgombea wa Chama cha CUF, Rajabu Salum Jimbo la Kinondoni na ndiye aliyemkaribisha kuzungumza kwenye ule msiba.
Amesema ni kawaida, yeye ni kiongozi na kwamba mtu yeyote anaweza akapiga picha nae hivyo kama kuna watu walitumia tofauti ni wao wenyewe.
"Huyu binti amekuwa akitukana sana kwenye mitandao amenutukana sana lakini amefika mahala amewatukana hadi waislamu, Mange Kimambi amekuwa ni jasiri sana kwamba mdomo wake ni mchafu na watu wamuogope.
"Leo nataka niseme jambo moja, Mange ametukana viongozi mbalimbali wa serikali hadi wa vyama mbalimbali ni kawaida yake....lakini alimtukana hata Mufti kwa Kumpongeza Rais John Magufuli.
"....Kitendo alichokifanya tunataka tumwambie na sauti hii hataisikia tena baada ya leo hatutamjibu...ulimi wake aliomuumba M/Mungu anautumia vibaya, mikono yake anaitumia vibaya kudhulumu heshma za watu.
Ameongeza kuwa amedhulumu heshma ya viongozi wa dini na kwamba watarejea kwenye mahakama ya mbinguni ambayo itajibu na kwamba hawamtishi.
"Hatumtishi kwamba huu utakuwa mwaka wake wa mwisho kutumia ulimi wake kuvunja heshma za watu... Hata kama mtu amekosea kuna kitabu gani kinasema atukanwe, "amesema.
Amesema dua ya mwenye kudhulumiwa mtu haina kizuizi na kwamba kama anaishi chini ya mbingu hatakuwa salama kwa kuvunja heshima za viongozi wa dini.
"Atukane wanasiasa wamvumilie...sisi tumefika mahala kwa hili hatuhitaji tena kuliendea kwa hekima,"amesema.
Amesema siku zake zinahesabika na kwamba Watanzania watashuhudia kutotukana tena na kuvunja heshma zao.
"Tunamtahadharisha na kumuonya acheze na namba nyingine na si za viongozi wa dini, tumechoka kutukanwa, "amesema.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.




No comments:
Post a Comment