Chadema wamkataa msimamizi uchaguzi Kinondoni, waituhumu CCM kuingiza mamluki105...soma habari kamili na matukio360..share

Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

CHAMA cha Chadema kimedai CCM imeleta mamluki zaidi ya 105 kutoka Zanzibar kuhujumu uchaguzi mdogo wa marudio wa ubunge Jimbo la Kinondoni  utakaofanyika Februari 17, 2018

Pia  Chadema imemkataa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni ikidai anaihujumu kwa makusudi.
Mkuu wa Operesheni ya Uchaguzi wa Chadema Benson Kigaila akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mwenendo wa uchaguzi Kinondoni.

Shutuma hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Operesheni ya Uchaguzi wa chama hicho ,Bensoni Kigaila akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa uchaguzi huo.

“Tumebaini kwa nia mbaya Jumamosi Februari 4, 2018 majira ya saa 4 asubuhi, CCM wameleta vijana kutoka Zanzibar kuja kufanya vurugu kwenye uchaguzi wa Kinondoni,” amesema Kigaila.

Kigaila amedai  watu hao wamegawanywa katika kambi tatu na wasambaziwa silaha aina ya panga, shoka na nondo.

Amedai  vijana wa Chadema jana majira ya saa 9 Alasir walishuhudia gari aina ya Toyota Cruzer rangi ya Cream T ... DGS(namba tumezihifadhi) likiwa na watu 10 wakishusha silaha hizo kwenye ofisi za CCM zilizopo katika viwanja vya Alimapilau.

Amesema vijana hao wa CCM wamehifadhiwa katika gesti na hoteli mbalimbali zilizopo kinondoni huku akieleza kuwa baadhi wamehifadhiwa katika gesti za kijitonyama, Mwananyamala na  80 wakiwa eneo la Vijana Magomeni.

Amesema kufuatia hali hiyo ni kwamba wamekwisha andika barua ya kupeleka madai hayo kwa Inspekta Jenerali wa polisi (IGP) kwa ajili ya kuchukua hatua ili fujo zisije kutokea.

Matukio360 ilimtafuta katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kuhusu tuhuma hizo, alijibu tuma ujumbe.

Alipotumiwa meseji hadi tunatoa habari hii hakujibu chochote.

Katika hatua nyingine Chadema imetangaza kumkataa msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Kinondoni kwa sababu kuu mbili.

Akitaja sababu hizo ni kwamba msimamizi huyo ameruhusu kwa makusudi au kwa kujua kuruhusu tuhuma za kijinai dhidi ya Chadema zilizotolewa na CCM kupelekwa kwenye kamati ya maadili kinyume na utaratibu.

Amesema katika tuhuma hizo ni kwamba CCM ilipeleka malalamiko kuwa Chadema ilikiuka maadili ya Uchaguzi kwa vijana wanaodawa kuwa ni wa chama hicho kumpiga kijana wa CCM huku ikijulikana kuwa swala hilo ni la jinai na lilitakiwa kupelekwa polisi.

Na sababu nyingine ya kumkataa ni msimamizi huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa makusudi ama kwa kutojua kuruhusu vikao vya kamati ya maadili kusimamiwa na mwenyekiti asiyetambulika na wajumbe.


Hivyo kigaila amedai  kutokana na sababu hizo wameona kuwa kuna hujuma za makusudi zinafanywa na msimamizi huyo kwenye uchaguzi hivyo kama akiachwa hawatafika salama.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search