Kiongozi upinzani Kenya ashtakiwa kwa uhaini ....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
KIONGOZI wa upinzani nchini Kenya, Miguna Miguna ameshtakiwa Kwa kosa la uhaini kufuatia kuhusika kwake katika kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.
Miguna Miguna akimuapisha Raila Odinga
Miguna alishtakiwa kwa kuhudhuria na kuidhinisha kiapo alichokula Raila, kushiriki katika mkutano uliokuwa kinyume na sheria na kuhusika na maswala ya kihalifu.
Amefikishwa katika mahakama ya kaunti ya Kajiado  maili 50 kusini mwa Nairobi
''Kwa mara nyingine serikali inakiuka haki za Miguna kwa kumsafirisha kutoka eneo moja hadi jingine bila ya kujulisha familia ama wakili wake," amesema  Okero ambaye ni wakili wakeM
Miguna angali katika mikono ya polisi huku akiwa hajulikani aliko licha ya kwamba mahakama ya Nairobi ilitaka aachiliwe kwa dhamana ya ksh. 50,000 siku ya Ijumaa.
Mnamo tarehe 30 mwezi Januari, Miguna alikuwa kiungo muhimu katika kumuapisha Raila Odinga kuwa rais wa wananchi katika bustani ya Uhuru Park jijini Nairobi.
Siku chache baadaye, mnamo  Februari 2, alikamatwa katika uvamizi wa alfajiri katika nyumba yake.
Viongozi wengine wawili wa upinzani pia walikamatwa.
Odinga na wafuasi wake walipinga matokeo ya uchaguzi wa mwaka uliopita ambao rais Uhuru Kenyatta alifanikiwa kushinda awamu ya pili katika uchaguzi wa marejeo mwezi Oktoba.
Kenyatta alihifadhi kiti chake kwa kupata asilimia 98 ya kura mnamo tarehe 26 Oktoba ikiwa ni asilimia 39 ya kura zote zilizopigwa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search