Chadema wamvaa Magufuli,kuishtaki serikali...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar
es Salaam
CHAMA cha Chadema kimemtaka rais John Magufuli kutoa kauli kuhusu watu 40
wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kinyume na sheria ikiwa wanashikiliwa kwa
agizo lake au la
Naibu katibu mkuu wa Chadema bara, John Mnyika
Pia kimelitaka jeshi la
polisi mapema leo kutoa dhamana au kuwafikisha mahakamani watu hao na endapo
litashishindwa kimedhamiria kuishtaki serikali ili
mahakama iweze kutoa haki ya kuwapatia dhamana.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, John Mnyika
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu watu 40 wanaoshikiliwana
jeshi la polisi kutokana na maandamano ya chama hicho kwa siku sita mfululizo
bila kupatiwa dhamana.
“Rais Magufuli ni vyema
akatoa kauli na waziri wa mambo ya ndani atoe kauli iwapo uamuzi wa jeshi la
polisi kuwashikilia watu wote hawa kinyume cha sheria mpaka hivi sasa ni agizo lililotolewa na rais Magufuli au
waziri wa mambo ya ndani,”
Mnyika amesema watu hao
wanashikiliwa katika kituo cha kati “Central”, Msimbazi na Ostabey.
Naibu katibu huyo
amesema miongoni mwa watu hao wawili wana majeraha ya risasi na hawajapatiwa
matibabu yanayostahili lakini pia kuna mzazi anayenyonyesha mtoto wa miezi minne
aliyeko katika kituo cha kati pamoja na kijana wa miaka 15 mwanafunzi.




No comments:
Post a Comment