Yanga yavutwa shati, Ajib atupia...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Yanga imetoshana nguvu na timu ya St. Louis ya
Shelisheli kwa kufungana goli 1-1 katika mchezo wa marudiano kwenye michuano ya
kombe la klabu bingwa barani Afrika uliochezwa nchini Shelishili.
Ibrahim Ajib
Yanga ndiyo ilikuwa ya kanza kupata goli lililofungwa na
kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib kunako dakika ya 45 kipindi cha kwanza huku la
St. Louis likifungwa kunako daika ya 90 kipindi cha pili.
Pamoja na matokeo hayo Yanga imefuzu hatua ya pili katika
mashindano hayo kwa jumla ya magoli 2-1.
Katika hatua ya pili Yanga anatarajwa kukutana na mshindi
kati ya Al Merriekh ya Sudan na Township Rollers ya Botswana.




No comments:
Post a Comment