Chelsea, Barcelona hakuna mbabe, Buyern Munich yaangamiza....soma habari kamili na matukio360...#share


Na mashirika ya kimataifa
CHELSEA na Barcelona zimetoshana nguvu kwa kufungana 1-1 huku Buyern Munich ikiichapa Besiktas 5-0 katika mechi za kwanza mzunguko wa 16 mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Messi bhana!!!!!

Lionel Messi akiwatoka wachezaji Chelsea

Kunako dakika ya 62 William aliiandikia Chelsea  bao la kuongoza lakini dakika 15 baadaye yaani dakika ya 75 Lionel  Messi aliisawazishia Barcelona. Alifunga kutokana na makosa yaliyofanywa beki wa Andreas Christensen.
Hata hivyo kocha wa Chelsea, Antonio Conte amemtetea beki huyo na anaamini timu yake itafanya vizuri katika mechi ya marudio katika uwanja wa Nou Coump, Hispania
Nayo Buyern imetoa kipigo cha mbwa mwizi cha bao 5-0, Thomas Muller alifungua idadi hiyo ya magoli. Aliingia nyavuni kunako dakika ya 43 na 66, Kingslyes Coman dakika 52 na Robert Lewandowsksi dakika 79 na 88

Muller akifunga goli

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search