TUICO yakemea rushwa ....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Mbeya

CHAMA cha Wafanyakazi wa Viwandani, Biashara, Taasisi za Fedha ,Huduma na Ushauri (TUICO)Mikoa ya nyanda za juu kusini, kimewataka Viongozi wa vyama vya wafanyakazi kukemea vitendo vya rushwa, ubadhilifu na ufisadi na kimewataka wafanyakazi kufanya kazi kwa tija ili kuleta mafanikio sehemu zao za kazi.




Daud Mpolya

Mwenyekiti wa TUICO Mikoa ya kanda ya Nyanda za juu kusini, Daud Mpolya amesema hayo katika mkutano mkuu wa mwaka
uliofanyika jijini Mbeya, kutathmini kazi na majukumu waliyojipangia  mwaka uliopita. Umeshirikisha vyama vya wafanyakazi mkoa wa  Iringa Mbeya na Rukwa.


“ Nawaomba viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi msimamie maadili, uaminifu, utendaji kazi wenye tija mahala pakazi, lakini pia vitendo vya ubadhilifu, ufisadi na rushwa mahala pa kazi havitakiwi," alisema mwenyekiti huyo.

Amewataka wafanyakazi wote kuungana na jitihada za rais Dk John Magufuli za kukemea vitendo viovu na kuanzisha viwanda vidogo.

Mwenyekiti wa TUICO Mkoa wa Mbeya Winfrida Mnandi aliwataka wafanyakazi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kazini kwa kuwahi na kufanya kazi kwa bidii.

“Mfanyakazi yeyote anatakiwa kufanya kazi kwa weledi na kujituma pamoja na kuwahi kazini, lakini ni vigumu kwa mfanyakazi ambaye hatimizi majukumu yake kudai haki hii haikubaliki, wapo baadhi ya wafanyakazi wanashindwa kutimiza majukumu yao ,na wanakuwa wa kwanza kualalamika kwenye vyama kuwa waajili wao hawawatendei haki, sasa muajiri atakupaje haki wakati hutimizi majukumu yako, naomba tutimize wajibu wetu,”alisema mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti wa TUICO Mkoa wa Rukwa Lwamo Shabani
Malanda ameiomba serikali kuwa karibu na wafanyakazi ili kufikia malengo ya kuijenga nchi.

Amesema serikali itekeleze majukumu yake kwa wafanyakazi kwa kuwalipa stahiki zao kwa wakati.

Katibu wa TUICO kanda hiyo, Merboth Kapinga alisema uwajibikaji kwa wafanyakazi unaoenda sambamba na usawa kwa wote, utasaidia kwa

kiasi kikubwa mfanyakazi kuwa na nguvu ya kudai haki ikiwemo mikataba mizuri kwa wa ajili.

“ Ikiwa kutakuwa na usawa kwenye utendajikazi kwa maana ya kwamba mfanyakazi akatimiza majukumu yake na mwajiri pia, hii itakuwa na nguvu hata kwa mfanyakazi kudai haki yake ya mkataba kwa kuwa ana uhakika amewajibika kazini kwake na kuleta tija."




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search