Ellen Sirleaf mshindi tuzo ya Mo Ibrahim....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa
RAIS wa zamani wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf ameshinda tuzo ya mwaka ya Mo Ibrahim kwa Uongozi wa Afrika - ambayo hupewa viongozi wa Afrika ambao wameonekana kuwa na utawala mzuri.
Ellen Johnson Sirleaf
Ellen Johnson Sirleaf amekuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya Urais mwaka 2006 na kumaliza muda wake mwezi uliopita baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.
Kamati ya Utendaji ya tuzo ya Mo Ibrahim imesema Ellen Johnson Sirleaf ameonesha uongozi wa kipekee katika kukabiliana na changamoto zisizowahi kutokea katika awamu zake mbili za uongozi alipokuwa Rais wa Liberia.
Wakati aliposhinda uchaguzi wa Rais nchini humo mwaka 2005, nchi hiyo ilikuwa imegawanyika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka kadhaa na tuzo hiyo ya amani ilikuwa ni kwa ajili ya kumpongeza kusaidia kuiimarisha nchi hiyo.
Wakosoaji wake wamekuwa wakimkosoa kwa kuwa na upendeleo, kutokana na kuwachagua watoto wake katika nafasi za ngazi za juu na pia wanadai kuwa hakuchukua hatua za kutosha kupambana na rushwa.

Kamati yab utendaji ya Mo Ibrahimu imearifu kwamba inafahamu mapungufu yake, lakini imeamua kwamba anastahili kupata tuzo ya dola za kimarekani milioni 5.
Mjasiriamali Mwingereza mwenye asili ya Sudan Mo Ibrahim alianzisha tuzo hiyo mwaka 2007 kwa ajili ya kuwatunukia viongozi walionesha kazi nzuri wakati wa kipindi cha uongozi wao ndani ya bara la Afrika, amballo madikteta na watawala wadhalimu wamerudisha nyuma maendeleo ya bara hili.
Tuzo hii ambayo inapaswa kutolewa kila mwaka , kwa mara sita mfululizo ilishindwa kupata mtu, kutokana na viongozi kukosa sifa za kushinda tuzo hiyo.
Ellen Johnson Sirleaf atapata dola za Kimarekani milioni tano zitakazogawanywa kwa miaka kumi, na dola laki mbili kwa maisha yake yote.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search