Jacob Zuma kung'olewa madarakani leo?....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
KIONGOZI wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC, Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa leo chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya rais Jacob Zuma.
Jacob Zuma

Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Cape Town jana, Ramaphosa amedokeza kuwa rais Zuma atatakiwa kujiuzulu.
Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa hilo angekitaka.
Ramaphosa alikuwa akizungumza katika kumbukumbu ya miaka 28 toka Rais wa kwanza mzalendo nchini humo Nelson Mandela alipolihutubia taifa, mara tu baada ya kuachiwa gerezani.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search