Jacob Zuma ajiuzulu....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa
HATIMAYE Jacob Zuma amejiuzulu urais wa nchi ya  Afrika  kusini.

Amejiuzulu jana usiku akiwa Ikulu, Pretoria. Amesema hatua yake hiyo imezingatia maslahi mapana ya wanachama wa ANC.
Jacob Zuma

Ameitumikia ANC kwa miaka 60. Zuma aliingia madarakani mwaka 2009. Chama chake cha ANC kimepokea uamuzi huo kwa furaha.

Sasa ANC inatarajia kupendekeza jina la rais mpya wa nchi hiyo ambaye atathibitishwa na Bunge la nchi hiyo.

Cyril Ramaphosa aliyechaguliwa kuwa rais wa chama hicho mwezi Disemba anatarajiwa kuwa rais wa taifa hilo.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search