Jalada kesi Aveva, Kaburu lapelekwa kwa DPP....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mwandishi wetu  Dar es Salaam. 

JALADA la kesi  inayowakabili viongozi wakuu wa klabu ya Simba Evans Aveva na Godfrey Nyange  limerejeshwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kupitiwa na kujiridhisha na upelelezi na mashtaka.


Aveva kushoto akiwa Kaburu

Leo mwendesha mashtaka mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai ameeleza hayo p kwa Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu,Victoria Nongwa.

Swai amedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na jalada limerudishwa kwa DPP ili kupitiwa na kwamba wanasubiri alipitie na kujiridhisha na upelelezi na mashtaka.

Wakati kesi hiyo ikitajwa mahakamani hapo alikuwapo Godfrey Nyange maarufu Kaburu ambaye ni makamu wa rais wa klabu ya Simba.

Swai amedai  rais wa klabu ya Simba Aveva hakufika mahakamani kwa sababu bado anaumwa na amepelekwa Hospitali katika kliniki yake.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, wakili wa utetezi, Steven Mwakiborwa aliomba kesi hiyo ipangiwe tarehe fupi.

Kesi imeahirishwa hadi Machi Mosi, 2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Washtakiwa hao, wanakabiliwa na Mashtaka matano ya  uhujumu uchumi ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha wa Dola za Marekani (USD) 300,000.

Washtakiwa hao wapo mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search