Tetesi za soka Ulaya leo Alhamisi....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger anamtaka mshambuliaji wa Uingereza Danny Welbeck, 27, kutia saini kandarasi mpya na Arsenal . (Daily Mail)

Danny Welbeck
Mchezaji wa zamani wa Newcastle na Tottenham, David Ginola amepata mtoto mwengine akiwa na umri wa miaka 51, ikiwa ni miaka miwili baada ya kupata mshutuko wa moyo wakati wa mechi ya hisani. (BirminghamLive)

Beki wa Tottenham Davinson Sanchez, 21, anasema kuwa hapendelei uhamisho wa kuelekea Real Madrid mwisho wa msimu huu .Raia huyo wa Colombia alijiunga na Spurs kutoka Ajax Agosti iliopita. (Mirror)
West Bromwich Albion inamchunguza meneja wa klabu ya Ostersunds Graham Potter. Raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 42 anasema kuwa anapanga kufunza katika ligi ya Uingereza katika siku za usoni. (Daily Mail)
Ajenti wa kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba amewasilisha ombi la kuhama la mchezaji huyo katika klabu kubwa za Ulaya .
Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 alianza mechi ya United ya 0-0 dhidi ya Sevilla siku ya Jumatano akicheza kama mchezaji wa ziada. (Sports Illustrated)
Real Madrid inamtaka kipa wa Chelsea Thibaut Courtois, 25, kuchelewesha kutia saini kandarasi yake mpya na klabu hiyo hadi mwezi Aprili ambapo watafanya uamuzi wa kumsajili raia huyo wa Ubelgiji ama kipa wa Man United David de Gea, 27. (Telegraph)
Courtois amekiri kwamba ajenti wake atasikiliza ombi kutoka timu hiyo ya La Liga.. (Mirror)
Klabu ya ligi ya kwanza ya Nantes nchini Ufaransa imesema kuwa haitamzuia meneja wake Claudio Ranieri iwapo atapewa wadhfa wa kocha mkuu wa Itali. (L'Equipe - in French)
Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema, 30, ananyatiwa na klabu nne za Ufaransa ikiwemo Lyon, Paris St-Germain lakini mchezaji huyo hapendelei kuondoka. (AS
Beki wa Uingereza Harry Maguire, 24, yuko tayari kumaliza soka yake katika klabu ya leicester , licha ya beki huyo anayedaiwa kuwa na thamani ya £50m kuhusishwa na uhamisho wa klabu ya Manchester City. (Sun)
Manchester United ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Dinamo Zagreb mwenye umri wa miaka 19 Nikola Moro, ambaye ametajwa kuwa 'Luka Modric mpya' (Talksport)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search