Jalada kesi mhasibu Takukuru lapelekwa kwa DPP... soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abdulrahim Sadiki,Dar es Salaam.
JALADA la kesi inayomkabili aliyekuwa mhasibu mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai anayedaiwa kumiliki mali zenye thamani ya Sh bilioni 3 ambazo haziendani na kipato chake limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Gugai akiwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam
Hatua hiyo imeelezwa leo na Wakili wa Serikali,Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba.
Wankyo ameeleza kuwa awali jalada hilo lilipelekwa kwa DPP, amelipitia na kulirejesha Takukuru na kuelekeza baadhi ya maeneo yafanyiwe uchunguzi zaidi.
Maeneo hayo yamekwisha fanyiwa kazi na jalada limerejeshwa tena kwa DPP kwa ajili ya kulipitia na kulitolea maamuzi.
Kufuatia maelezo hayo Wankyo aliiomba mahakama iipangie kesi hiyo tarehe nyingine ili waweze kueleza hali ya upelelezi ikoje.
Kwa upande wa mshtakiwa Gugai alidai sasa wamefikisha siku 90 na akaomba kesi ipangiwe siku saba ili waweze kujua hali ya upelelezi ikoje.
Hakimu Simba ameahirisha kesi hadi Februari 21,2018 na kuutaka upande wa mashtaka uhakikishe wanalifanyia kazi jalada hilo kwa kuwa limeanza kuwa zee.
Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera
Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.
Gugai na wenzake wanasota mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment