Magufuli awatunuku kamisheni maafisa 197 wapya JWTZ....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

RAIS John Magufuli ambaye pia ni amir jeshi mkuu, leo Februari 3, 2018 amewatunuku kamisheni maafisa wapya  197 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).



Rais na Amir Jeshi mkuu wa Tanzania, Dk John Magufuli akitunuku kamisheni

Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam na wamekuwa maafisa Luteni usu.  Kati ya hao, wanawake ni 28.

Waliotunukiwa  kamisheni ni maafisa wa Jeshi la JWTZ kutoka Tanzania na nchi marafiki waliopata mafunzo  katika chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli mkoani Arusha

Kozi hiyo ilianza Januari, 2017 ikiwa na jumla ya wanajeshi 221 huku idadi ya wanajeshi kutokana nchi marafiki wakiwa ni 25. Miongoni mwa  nchi hizo ni Uganda na Burundi.

Hii ni mara ya tano kwa rais Magufuli kutunuku kamisheni kwa wanajeshi wa JWTZ tangu aingie madarakani Novemba 2015

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search