Magufuli azuia kuondolewa kaya 1,900 Mwanza...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
RAIS John Magufuli amezuia kuondolewa kaya zaidi 1,900 zinazoishi katika nyumba zilizopo karibu na uwanja wa ndege wa Mwanza hadi serikali itakapofanya tathimini yakufidia wananchi hao.
Rais John Magufuli alipowasili katika uwanja wa ndege jijini Mwanza akitokea nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa maris wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Ametoa zuio hilo jana baada ya kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa Uwanja huo ambao walimweleza Kuwepo kwa kaya hizo ambazo zinakwamisha ujenzi wa uwanja.
“Hawa watu ndiyo walionipa kura, msiwaondoe hadi pale mtakapokamilisha kuwalipa madai yao,” amesema rais Magufuli.
Oktoba mwaka jana, rais Magufuli aliagiza kusitishwa kwa ubomoaji wa nyumba za wananchi zaidi ya 2,000 wanaodaiwa kuvamia eneo la uwanja huo, kituo cha polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Naye Meneja wa uwanja, Ester Mandale alimweleza rais kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa jengo la wasafiri, uwanja kukosa uzio pamoja na ndege kuzuiwa kubeba samaki.
Amesema baada ya ndege kuzuiwa kusafirisha samaki kwenda nchi za nje, wanalazimika kusafirisha kwa kutumia magari wakati wenzao wa Kenya wanatumia ndege, hivyo kuikosesha Serikali mapato.
Akizungumzia changamoto hiyo, rais Magufuli amemwagiza meneja huyo kufanya tathmini inayohitajika Katika Ujenzi wa Jengo la Usafiri Pamoja na Uzio kisha Aiwasilishe Serikalini Kwa ajili Ya kuanza ujenzi Huo.
Rais aliondoka jijini Mwanza na kuelekea Chato kwa ajili ya mapumziko.
No comments:
Post a Comment