Zitto ataka mkutano wa maridhiano...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Arusha
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ametaka kuitishwa kwa mkutano wa kitaifa wa maridhiano ya kisiasa nchini.
Kiongozi wa Chama cha ACT wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana,kuhusu hali ya kisiasa nchini na matukio ya kihalifu yanayoendelea kutokea.
Kiongozi wa Chama cha ACT wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana,kuhusu hali ya kisiasa nchini na matukio ya kihalifu yanayoendelea kutokea.
Amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, amesema mkutano huo utalenga kujadili changamoto zote za uendeshaji wa siasa nchini na kukubaliana kanuni za demokrasia ya vyama vingi.
"Hii ni kutokana na dhahiri kwamba mfumo wa vyama vingi nchini upo hatarini zaidi kuliko wakati wowote," amesema Zitto.
Zitto amesema wadau wanaoweza kufanikisha mkutano huo ni asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wafanyabiashara, na vyama vya wakulima na wafugaji.
Amesema hali ya kisiasa ya sasa nchini siyo ya kuachia wanasiasa peke yake maana sasa inahusu uhai wa watu na wengine wasio jihusisha na siasa.
No comments:
Post a Comment