Mbunge Mwakajoka awekwa mahabusu....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Tunduma

MBUNGE wa Tunduma, wilayani Momba mkoani Songwe(Chadema), Frank Mwakajoka amekamatwa na polisi kisha kuwekwa mahabasu kwa saa 48 Kwa kinachodaiwa ni amri ya mkuu wa wiilaya hiyo, Jumaa Irando

Hatua hiyo inadaiwa ni mbunge huyo kuwahamasisha wananchi wasichangie michango ya ujenzi wa zahanati moja kwa kuwa tayari serikali imetenga fedha za ujenzi huo.

Frank Mwakajoka

Mwakajoka amekamatwa akiwa njiani akienda katika shughuli zake baada ya kuhudhuria kikao cha madiwani.


Hii ni mara ya pili kwa Mbunge Mwakajoka kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa saa 48 kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya. Agosti mwaka jana Irando aliamuru kukamatwa Mwakajoka kwa kile alichodai alitoa lugha ya kumdhalilisha yeye na Serikali ya Mkoa wa Songwe wakati akiwa kwenye mkutano wa hadhara.









About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search