Waziri Mbarawa alia na wakandarasi wazawa....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Tabora
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka wakandarasi wazawa wa kampuni ya Samota, Anam na Jossam JV wanaojenga barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 kwa kiwango cha lami wakamilishe ujenzi wa barabara hiyo kwa muda uliowekwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri (kushoto), alipomtembelea ofisini kwake katika ziara yake ya kikazi mkoani humo kwa lengo la kukagua miradi ya ujenzi ya barabara iliyokamilika na inayoendelea. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Queen Mlozi.
Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo katika kijiji cha Motomoto, Wilaya ya Urambo mkoani Tabora alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua mtandao wa barabara mkoani humo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo.
“Nataka nione kazi za ujenzi zinafanyika kwa haraka, kwani uzoefu unaonesha baadhi ya wakandarasi wazawa wamekuwa na kasi ndogo, hivyo mjipange vizuri ili barabara ikamilike kwa wakati," amesema Prof. Mbarawa.
Amesema nia ya Serikali ni kuwajengea wakandarasi wazawa uwezo ili waweze kutekeleza miradi mikubwa mingine ya ujenzi nchini lakini haitasita kuwanyima kazi hizo kama miradi hiyo itacheleweshwa, haitakidhi viwango vinavyohitajika na kama hawataonekana eneo la kazi kwa kipindi kirefu.
“Mkandarasi mzawa atakayechelewesha mradi wowote wa ujenzi hatapewa kazi nyingine kwa sababu atakuwa amechelewesha maendeleo ya wananchi," amesisitiza Prof. Mbarawa.
Amesema serikali imejipanga kuwalipa wakandarasi wazawa kwa wakati ili waweze kutekeleza miradi yao kwa ufanisi.
Mbunge wa jimbo la Urambo, Magreth Sitta, amemueleza Waziri Prof. Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi wa wilaya yake na Kaliua na hata mikoa jirani kwa kuwa usafirishaji wa mazao na abiria utarahisishwa.
Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Kwingwa amesema wamejipanga vyema kutoa ushirikiano kwa wakandarasi wazawa na kuahidi kumsimamia ili amalize kazi hiyo kwa wakati, lakini kwa kiwango.
Awali akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa barabara hiyo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo Mhandisi Damian Ndibalinze amesema mkandarasi ameshapewa fedha za mradi hivyo hakuna sababu ya kuchelewesha mradi huo na kuahidi kuwasimamia ili wakamilishe kabla ya mwaka 2020.
Ameongeza ujenzi wa barabara hiyo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 37.6 na zote zikiwa zinafadhiliwa na serikali kwa asilimia 100.
Katika hatua nyingine, Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Tabora-Pangale yenye urefu wa KM 30 inayojegwa na mkandarasi CICO kwa gharama ya shilingi bilioni 28.6 na kumtaka mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi wa sita.
Waziri Prof. Mbarawa yuko mkoani Tabora kwa ziara ya siku mbili akiwa na lengo la kukagua utekelezaji wa miundombinu ya barabara, mkoani humo

No comments:
Post a Comment