Mtanzania akamatwa na dhahabu dola milion moja... soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa
MAAFISA  forodha nchini Kenya wamemkamata Abdallah Abdi anayedaiwa kuwa raia wa Tanzania katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi akisafirisha dhahabu ya thamani ya dola milioni moja.
Vipande hivyo vya dhahabu vya uzani wa kilo 32.3 vinashikiliwa na maafisa wa idara ya forodha wa KRA huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 46 anadaiwa kuwasili kutoka Mwanza, Tanzania kupitia uwanja wa Kilimanjaro na alikuwa safarini kuelekea Dubai.
Gazeti la kibinafsi ya Nation linasema mwanamume huyo, ambaye jina lake halijafichuliwa kufikia sasa, aliwasili uwanja wa JKIA Ijumaa 16 Februari kwa ndege ya Precisio Airlines na alitaka kusafiri kwa ndege ya Kenya Airways kuelekea Dubai.
Maafisa wa idara ya Uchunguzi wa Jinai wakiandamana na maafisa wa uchunguzi kutoka Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) walimhoji na akaandikisha taarifa.

Sheria za Usimamizi wa Forodha za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za mwaka 2004, kKifungu 85(3) na Kiambatisho cha Pili Sehemu B (4) huharamisha usafirishaji wa madini ambayo hayajapitia viwandani katika kanda ya Afrika Mashariki.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search