Asasi za kiraia wapendekeza mambo 15 serikalini...soma habari kamili na matukio360....#share
Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
WAKURUGENZI wa Asasi Kiraia nchini wametoa wito wa mapendekezo 15 kwa Serikali kuhusu hali ya usalama wa raia, haki za binadamu na utawala wa sheria nchini.
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa akisisitiza jambo kwa wanahabari wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Asasi za Kiraia nchini na wanahabari. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Paul Mikongoti.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kwa vitendo vya kutekwa, kuuawa, kuumizwa na kupotea kwa watu mbalimbali, matumizi ya sheria kandamizi na ukamataji usiozingatia sheria, hali ya watetezi wa haki za binadamu na Azaki.
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema serikali itazame upya suala la upatikanaji wa katiba mpya na ndiyo suluhisho la matatizo mbali mbali yanayotokea katika jamii kwa sasa.
"Tunashauri mchakato wa katiba mpya ufanyike mwaka huu kwa kuwa mwaka 2019 na 2020 taifa litakuwa 'bize' na mambo ya uchaguzi. Tunamshauri Rais aitishe kikao cha wadau wote kujadili namna ya kuliweka hili suala kwa maslahi ya taifa,"amesema.
Amesema wanaomba Tume Huru ya Uchaguzi ipatikane kabla ya chaguzi za 2019 na 2020,itakayoweza kusimamia usawa na haki kwa vyama vyote kuepusha madhara ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na tume kushindwa kusimamia misingi ya haki na usawa katika uchaguzi.
"Tume ya uchaguzi ifungue ofisi zake wilayani na kuajiri wataalam wake kuwa wasimamizi wa uchaguzi na kuachana na mfumo wa sasa unaonekana kuwa na mgongano wa kimaslahi,"amesema
Amefafanua kuwa "Tunapendekeza iundwe tume huru ya uchunguzi itakayohusisha AZAKI, Taasisi za Dini, Vyombo vya Habari, Baraza la Vyama vya Siasa, Wanahabari, Majaji/Mahakimu, Polisi, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora kufanya uchunguzi huru juu ya vifo na vitendo vya utekwaji na utesaji vilivyojitokeza wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni,"amesema.
Ameongeza matukio yanayowahusu Polisi kama watuhumiwa ni kosa kuwaachia wao wenyewe wajichunguze jambo linalosababisha kuwa chanzo cha matukio kuendelea kutokea na kutochukuliwa hatua.
Olengurumwa amesema vyombo vya utoaji haki kama Polisi na Mahakama vifanyiwe maboresho na viachiwe viwe huru katika kutekeleza majukumu yao ili kuepusha wasiwasi na dhana ya kutokuwa huru.
"Tunalisihi na kulishauri Jeshi la polisi kutimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa weledi,taaluma na sheria za nchi pamoja na kuacha kuegemea upande mmoja ili kuepusha lawama chuki na uhasama ambao unajengeka kwa wananchi kwa Jeshi hilo.
"Jeshi la polisi liwe makini katika kutimiza wajibu wake wakati wa kuzuia maandamano,kwani kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi wa Jeshi la Polisi na matumizi ya
silaha za moto huonesha wazi kwamba Polisi inashindwa kutumia njia zilizoanishwa kisheria kukabiliana na waandamanaji wasio na silaha na wasiofanya vurugu,"amesema.
Amesema askari wanaotuhumiwa kuhusika kusababisha kifo cha Mwanafunzi Akwilina wafikishwe katika vyombo vya sheria ili hatua stahiki zichukuliwe kwa aliyehusika na tukio hilo na kwamba kuwe na mfumo huru au chombo huru (Oversite body) ya kuchunguza na kusimamia mashtaka yanayohusu vyombo vya usalama badala ya kuwaachia wao kufanya uchunguzi na kuendesha mashtaka.
Ameongeza kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni ajipime mwenyewe kama anastahili kuendelea katika nafasi hizo kutokana na vitendo vyake alivyofanya katika uchaguzi mdogo uliofanyika Febuari 17/2018,kuvuruga taratibu za uchaguzi na kuwanyima mawakala wa vyama vingine haki ya kusimamia uchaguzi na kusababisha uvunjifu wa amani.
Olengurumwa amefafanua kuwa Tume ya Utawala Bora na haki za binadamu iingilie kati vitendo vya uvunjifu wa
haki za binadamu kwa kufanya utafiti huru juu ya yale yanayotokea katika jamii na kupendekeza njia sahihi za kushuhulikia ukiukwaji wa haki za binadamu.
"Tunaziomba asasi za kiraia, asasi za kiserikali, wabunge, wanasiasa, mashirika mengine na wadau mbali mbali wa maendeleo kuendelea kupaza sauti na kuungana kwa pamoja kupigania haki, utawala

No comments:
Post a Comment