Mwanasiasa Tambwe Hizza afariki dunia....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
MWANASIASA wa siku nyingi, Tambwe Hizza amefariki leo alfajiri nyumbani kwake jijini Dar es salaam.
Tambwe Hizza
Mmoja wa wanafamilia ameiambia matukio360 kuwa Hizza amefariki akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu na amefariki akiwa ni mmoja wa waratibu wa kampeni za chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika jimbo la Kinondoni.
" Hizza Tambwe amefariki usiku wa kuamkia leo, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu kwa muda mrefu, taarifa kamili za mazishi zitatolewa baadae," amesema
" Hizza Tambwe amefariki usiku wa kuamkia leo, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu kwa muda mrefu, taarifa kamili za mazishi zitatolewa baadae," amesema
Kabla ya kuipigia debe Chadema, Hizza alikuwa ni kiongozi mwandamizi wa chama cha CUF baadae iling'atuka na kujiunga CCM.
Umaarufu wake uliongezeka mwaka 2005 na 2010 alipogombea ubunge katika jimbo la Temeke jijini Dar es salaam kwa tiketi ya CUF
Umaarufu wake uliongezeka mwaka 2005 na 2010 alipogombea ubunge katika jimbo la Temeke jijini Dar es salaam kwa tiketi ya CUF
Kwa mara ya kwanza aliibuka na kuipigia debe Chadema kwa mwamvuli wa Ukawa kwenye ufunguzi wa kampeni wa uchaguzi mkuu mwaka 2015.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment