Tetesi za soka Ulaya leo Alhamisi....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola hatoanzisha tena harakati za kutaka kumsajili winga wa Leicester raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 26, Riyad Mahrez mwishoni mwa msimu huu. (mirror)
Riyad Mahrez
Liverpool inajiandaa kwa jaribio la pili kumsajili kiungo wa wakti wa Monaco mwenye umri wa miaka 22 Thomas Lemar wa Ufaransa baada ya kukataa kandarasi mpya katika klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza.
Mkufunzi wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ambaye anahusishwa na kuchukua mahala pake Antonio Conte wa Chelsea anajiandaa kuelekea nchini Uingereza.
Hata hivyo mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 47 hataki kumrithi Conte hadi mwisho wa msimu huu.
Tottenham inataka kumsaini kiungo wa kati wa Watford na Ufaransa Abdoulaye Doucoure mwishoni mwa msimu huu.
Beki wa Brazil, Fabinho mwenye umri wa miaka 24 ambaye klabu ya Manchester United ilikuwa inamnyatia msimu uliopita anasema kuwa muda wake katika klabu ya Monaco unakamilika(Metro)
Klabu ya ligu kuu nchini China Hebei China Fortune inajiandaa kuwasilisha ombi jingine kwa mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi, 30, baada ya ombi lao la kwanza kukataliwa. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk Fred amechagua klabu ya Manchester City kama klabu anayopanga kuhamia , kulingana na mkufunzi wa zamani Mircea Lucescu.
Raia huyo wa Brazil mwenye umri wa 24 pia amehusishwa na majirani wa City Manchester United. (Mirror)
Mshambuliaji wa Itali Fabio Borini na winga wa Uholanzi Jeremain Lens wataondoka Sunderland mwisho wa msimu huu baada ya kubadilisha vifungu vya sheria katika mkataba wao ambapo vinalazimu klabu zilizowasajili kwa mkataba wa muda kuwanunua.
Wako katika mkopo katika klabu za AC Milan na Besikitas mtawalia. (Northern Echo)
Nottingham Forest inajiandaa kumsajili kipa wa Ugiriki Stefanos Kapino. Mchezaji huyo mwnye umri wa miaka 23 aliondoka katika klabu ya Olympiakos iliokuwa ikimilikiwa na mmiliki wa sasa wa klabu ya Forest Angelos Marinakis baada ya migogoro kadhaa (Sun)
Mshambuliaji Benik Afobe, 24, atarudi katika klabu ya Wolvehampton kwa kandarasi ya kudumu iwapo viongozi hao wa ligi ya daraja la kwanza Uingereza watapandishwa katika ligi ya Premia.
Aliondoka katika klabu ya Molineux ili kujiunga na Bournemouth mwezi Januari 2016 lakini akarudi kwa mkopo mwezi Januari. (mirror)
Mshambuliaji wa Arsenal Striker Pierre-Emerick Aubameyang, 28, anasema kuwa alijiunga na Arsenal mwezi Januari baada ya kupigiwa simu na mchezaji wa zamani wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Ureno na Real Madrid Cristiano Ronaldo, 33, anasema kuwa anaweza kuendelea kucheza kwa kipindi cha muda mrefu ujao.. (GQ - in Italian)
Beki wa Manchester United Luke Shaw anatarajiwa kutia saini kandarasi mpya mwishoni mwa msimu huu.
Arsenal imeanza mazungumzo na kiungo wa kati Ainsley Maitland-Niles kuhusu mkataba mpya. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kutolka uingereza amesalia na miezi 18 mkataba wake kukamilika. (ESPN)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search