Profesa Bisanda awaasa vijana nchini....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
VIJANA wametakiwa kuwa
na fikra, mtazamo chanya kwenye uwajibikaji
ili kutambua nafasi waliyonayo katika kutumia fursa zilizopo nchini ili kujiletea maendeleo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Profesa Elifas Bisanda (kulia) na Mkurugenzi wa IYF Profesa Seong Hun Kim (kushoto) wakisaini makubaliano ya utoaji elimu ya kubadili fikra kwa wanafunzi wa chuo hicho.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Elifas Bisanda wakati wa utilianaji saini makubaliano ya ushirikiano baini ya chuo hicho na IYF (International Youth Fellowship) kutoka Korea Kusini kwa ajili ya kutoa elimu ya kubadili fikra kwa wanafunzi.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Elifas Bisanda wakati wa utilianaji saini makubaliano ya ushirikiano baini ya chuo hicho na IYF (International Youth Fellowship) kutoka Korea Kusini kwa ajili ya kutoa elimu ya kubadili fikra kwa wanafunzi.
“Tunahitaji vijana wa taifa
hili waanze kuwajibika na kutambua kwamba wananafasi kubwa ya kuleta
maendeleo pale walipo kwa kutumia fursa zilizopo,” amesema Prof. Bisanda.
“Haiwezekani nchi kama Tanzania
ambayo bado inaardhi kubwa isiyo na watu, inayofaa kwa kilimo, ufugaji na
utalii lakini vijana wanakimbilia mijini ambako hakuna kazi,” ameongeza.
Akizungumzia kuhusu
makubaliano hayo, Profesa Bisanda amesema IYF itasaidia kuleta walimu nchini watakaofundisha elimu ya kubadili fikra.
Amesema faida ya elimu
hiyo inasaidi kufanya mambo katika maisha kwa utaratibu, lakini pia inamfanya mtu
kujua umuhimu wa kuwajibika katika kujishughulisha na masuala ambayo
yatamsaidia binafsi na jamii.
“Leo hii katika nchi
yetu tuna tatizo la ajira, vijana wengi wakimaliza vyuo wanakaa tu, wanasema tunasubiri
kupata kazi, lakini si hivyo katika nchi zingine, vijana wa leo wanachagua
kazi, hivyo mawazo tuliyonayo watanzania inatakiwa fikra zibadilike, inatakiwa
kujifunza maarifa mapya na mbadala,” amesema.
Mkurugenzi wa IYF Profesa Seong Hun Kim, amesema wanafunzi wa chuo kikuu Huria cha Tanzania pia watapata fursa ya kushiriki katika kambi za vijana za kimataifa zinazofanyika kila mwaka mwezi Julai.
“Sisi tulianza
kuwekeza katika kulea watu na pia kufanya kampeni kupitia serikali
kuhusu mabadiliko ya fikra na mitazamo yao. Kupitia mafanikio na uzoefu
wa Korea Kusini unaweza kusaidia Tanzania
kwa kupitia mikutano na makongamano mbalimbali,” amesema Prof. Kim.
No comments:
Post a Comment