Kesi za maombi ya talaka zaongezeka Zanzibar....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
NAIBU Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora visiwani Zanzibar, Khamis Maalim amesema takwimu za mwaka 2017 zinaonesha kesi za madai ya talaka zimeongezeka katika mahakama za kadhi Unguja na Pemba ikilinganishwa na kesi za madai ya matunzo ya watoto.
Amesema kwa upande wa madai ya talaka takwimu zinaonesha kesi 884 zimefunguliwa Unguja na 440 zimetolewa uamuzi na kesi 444 zinazendelea kwa Pemba kesi 334 zilifunguliwa na kesi 249 zimetolewa uamuzi na 85 zinaendelea.
Katika kesi za madai ya matunzo ya watoto takwimu zinaonesha kesi zilizoripotiwa Unguja ni 35 kesi 17 zimetolewa uamuzi na 18
zinaendelea na kisiwani Pemba 22 zimefunguliwa 18 zimetolewa
uamuzi na nne zinaendelea.
Kauli hiyo aliitoa katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wakati
akijibu suali la mwakilishi wa jimbo la Konde Omar Seif Abeid huko Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Katika swali lake hilo mwakilishi huyo alitaka kujuwa kwa nini
Serikali haioni sababu ya kuweka sheria itakayoweza kuzilinda ndoa zisivunjike ovyo kama ilivyokuwa kwa wazee wa zamani.
Amesema kazi kubwa ya mahakama ni kupokea kesi na kutoa uamuzi kwa kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa na si vinginevyo na kuwa hakuna mamlaka au sheria yoyote ile iliyoipa mahakama kusajili ndoa au talaka.
“Uozeshwaji wa ndoa Zanzibar hufanywa na wasajili wa ndoa kwa mujibu wa sheria kwamfano masheikhe, makadhi, mapadri na watendaji wakuu wa mikoa,"amesema.
Alifahamisha kwamba uozeshaji huo hufanyika maeneo tofauti, ambapo mahakama haihusishwi katika uozeshaji na usajili wa ndoa hizo.
Hata hivyo amesema kutokana Zanzibar kuwa na idadi kubwa ya waislam itakuwa ni vigumu kuweka sheria itakayomzuia mwanandoa(mume) kutoa talaka na itakuwa inaenda kinyume na sheria zilizowekwa kiislamu
Hata hivyo amesema ili kulinda ndoa zisivunjike ovyo ni jukumu
la jamii nzima kuelimisha wanandoa waweze kustahamiliana katika ndoa ndoa.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na
Utawala Bora visiwani Zanzibar, Khamis Juma Maalim akijibu maswali yalioulizwa ndani
ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi linaloendelea Chukwani Mjini
Zanzibar.

About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment