Samia awataka skauti kushiriki shughuli za uzalishaji mali...soma habari kamili na matukio360...share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MAKAMU wa rais Samia Suluhu Hassan
amewataka Skauti nchini Tanzania kushiriki katika shughuli za Uzalishaji mali
kwa lengo la kujiongezea kipato na kukabiliana na changamoto ya Ukosefu wa
Ajira hasa kwa Vijana.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde akifungua mkutano mkuu wa Skauti Tanzania mjini Dodoma.
Hayo yamesemwa leo Mkoani Dodoma katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Skauti
Nchini ambapo akisoma hotuba ya makamu wa rais Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana
na Ajira Anthony Mavunde ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Katika hotuba hiyo, makamu wa rais amewapongeza skauti kwa
kushiriki katika matukio ya kijamii ikiwemo wakati wa maafa Kilosa na Pugu
kwenye machimbo.
Aidha amewataka skauti kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba Amani na
Mshikamano wa nchi unalindwa kwa nguvu zote.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, makamu wa rais wa Skauti Tanzania Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry amebainisha mipango mbalimbali ya
Skauti Tanzania katika kujiletea maendeleo na pia amemhakikishia mgeni rasmi
kwamba Skauti Tanzania itaendelea kujikita katika kusimamia HAKI, USAWA na
UZALENDO pamoja na kuhimiza AMANI na MSHIKAMANO miongoni mwa Watanzania.
Mkutano huo mkuu wa skauti agenda yake kuu ni Uchaguzi wa Uongozi wa
Skauti na Wajumbe wa Bodi.
Kwasasa sasa Skauti Tanzania ipo chini ya Uongozi wa Skauti Mkuu Mama
Mwantumu Mahiza na Kamishna Mkuu Abdulkarim Esmail Shah.
No comments:
Post a Comment