Simba yashinda, Okwi tena.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Gendarmerie ya Djibout katika mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho barani Afrika uliochezwa nchini Djibout.


Emanuel Okwi

Goli la Simba limefungwa na mshambuliaji Emmanuel Okwi dakika ya 55 kipindi chapili. Na kwa matokeo hayo wekundu hao wa Msimbazi wanasonga hatua ya pili ya mashindano kwa jumla ya magoli 5-0.

Itakumbukwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ilishindwa magoli 4-0 yalifungwa na John Bocco aliyefunga mawili, Emmanuel Okwi moja na Said Ndemla moja.

Hivyo katika hatua inayofuata Simba itakutana na klabu ya Al-Masry ya nchini Misri .

Kikosi kilichocheza cha Simba




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search