Wadaiwa SIDO wapewa siku 14....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
KAMPUNI ya udalali ya Yono Auction
Mart imetoa siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo
(SIDO), kulipa madeni yao kabla ya chukuliwa hatua za kisheria ikiwamo mali zao kupigwa mnada kufidia deni.
Meneja wa SIDO mkoa wa Dar es Salaam Macdonald Maganga akizungumza na waandishi wa habari.
Hatua hiyo imetangazwa leo
jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Scholastica Kevela
akizungumza na waandishi wa habari wakati SIDO ilipokuwa ikizindua kampeni ya
kukusanya madeni kwa wateja wao.
“Kwa wadaiwa wote
wa SIDO, wanaoishi kwenye viwanda na nyumba za SIDO bila kulipa pango,
waliochukua mikopo na hawataki kurejesha kwa sababu wanazozijua wao, mkono wa
Yono uko kazini ni vyema wakachukua hatua wakalipa ili kuondosha usumbufu,” amesema Kevela.
Meneja wa SIDO mkoani Dar es salaam, Macdonald Maganga amesema wadaiwa ni wale waliopewa maeneo maalumu ya viwanda kwa ajili ya kufanyia kazi zao na waliopatiwa huduma ya fedha kwa mkopo na kushindwa kurejesha kwa wakati.
“Kuna ambao wamekaa
miaka mingi au miezi mingi bila kurejesha fedha kwetu kama shirika
inatuathiri kwa sababu hatuwezi kuwahudumia wengine,” amesema Maganga.
Maganga amesema wanadai
jumla ya sh.milioni 350 kutoka kwa wadaiwa zaidi ya 77.
Mdaiwa Masoud amedai hawafanyi makusudi kutolipa madeni ni kutokana na kodi kupanda kila mwaka huku hali ya biashara ikiwa mbaya.
“Ukizingitia soko la
ushidani na hali ya bidhaa unashindwa kuuza kwa wakati kwa hiyo tunalipa lakini
hatulipi kwa wakati,” amesema.
Amedai wamepangishwa kwa zaidi ya miaka 40 wakifanya shughuli zao na kama wangekuwa hawalipi kwa kipindi chote wangefukuzwa hivyo
ameiomba serikali kutodhani kuwa wanapuuza kulipa madeni.
No comments:
Post a Comment