Tetesi za soka Ulaya leo Jumatano....soma habari kamili na matuki360....#share
Na mashirika vya kimataifa
Aliyekuwa mkufunzi wa Barcelona Luis Enrique ni miongoni mwa makocha walioorodheshwa na mmiliki wa timu ya Chelsea, Roman Abrahamovic kuchukua nafasi ya mkufunzi wa sass wa Chelsea Antonio Conte iwapo atafutwa kazi. (Sport - in Spanish)
Luis Enrique
Enrique ambaye ni raia wa Uhispania inadaiwa atamsajili mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez iwapo atasajiliwa kuifunza The Blues. (Le10Sport - in French)
Hatahivyo, Enrique hayuko tayari kukatiza likizo yake na kwamba yuko tayari kuchukua kazi hiyo mwisho wa msimu huu.(Goal)
Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte analipia makosa yaliofanywa na mkurugenzi wa zamani wa kiufundi katika klabu hiyo Michael Emenalo katika dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu uliopita kulingana na mchezaji wa zamani na naibu mkufunzi Ray Wilkins. (talksport)
Conte amesalia na miezi 18 katika kandarasi yake na kwamba hatowacha kazi (Mirror)
Abramovich hatoruhusu wachezaji kuamua iwapo Conte anfaa kusalia katika uwanja wa Stamford Bridge. (Telegraph)
Kipa wa Chelsea na Ubelgiji Thibaut Courtois, 25, anasema hali yake huenda ikamruhusu kuelekea klabu ya Real Madrid iwapo mabingwa hao wa Ulaya wataonyessha hamu ya kutaka kumsajili. (Sport Foot Magazine, via Daily Mail)
Kipa wa Manchester United David de Gea atasalia kuwa kivutio kwa Real Madrid' katika dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu, lakini United inatarajiwa kumpatia raia huyo wa Uhispania mkataba mpya. (Sport - in Spanish)
Arsenal wana hamu ya kumsajili beki wa Juventus Daniele Rugani, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo wa miaka 23 kutoka Itali. (Star)
Liverpool Itamtoa kwa mkopo beki wa Colombia mwenye umri wa miaka 18 Anderson Arroyo kwenda Real Mallorca baada ya kupokea nakala za kukamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya Fortaleza CEIF. (Liverpool Echo)
Kipa wa Roma Alisson, anayelengwa na Liverpool, ni kipa bora zaidi duniani na raia huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 ana thamani ya Yuro 50m kulingana na kocha Roberto Negrsolo. (Il Romanista, via Goal)
Klabu ya Benevento, ambayo iko pointi tisa chini ya ligi ya Serie A , imefanya majaribio ya kuwasajili aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Samir Nasri na Alex Song, wote wakiwa na umri wa 30, na wako huru. (Sky Italia - in Italian)
No comments:
Post a Comment