Waziri ateketeza eka sita za bangi ...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Arusha

WAZIRI wa mambo ya ndani nchini, Dkt Mwigulu Nchemba leo ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya ekari sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Waziri wa mambo ya ndani nchini, Dk. Mwigulu Nchemba leo ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya ekari sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Dk. Nchemba akishirikiana na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha,(RPC) Charles Mkumbo pamoja na vikosi vya askari wa jeshi la polisi mkoani hapa walilazimika kuacha magari yao njiani na kutembea umbali wa kilomita 5 milimani kufika katikati ya msitu huo ambapo wamiliki wa mashamba hayo walitokomea kusikojulikana.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo Mwigulu alisema kwamba  serikali itaendelea na oparesheni pande zote za nchi na haitasita kuwakamata wahusika wote na kutaifisha magari yatakayotumika kusafirisha bangi.


Mbali na kuwapongeza askari walioshiriki katika zoezi hilo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuteketeza  dawa za kulevya shambani, amewataka waongeze juhudi pia katika kupambana na madawa ya kulevya yanayotengenezwa viwandani.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search