Watu 250 wauawa Syria...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
IDADI ya watu waliokufa katika mashambulizi ya anga yanayotekelezwa na vikosi vya serikali katika mji Ghouta mashariki nchini Syria imefikia 250 kati ya idadi hiyo 50 ni watoto.
Baadhi ya watoto wakiokolewa kufuatia mashambulizi yanayoendelea katika mji was Ghouta, Syria
Umoja wa mataifa nchini Syria umesema una mashaka makubwa juu maisha ya mamia ya raia ambao bado wapo katika eneo linalolengwa na mashambulizi ya anga ya vikosi vya serikali ya Syria katika eneo la Ghouta mashariki.
Mashambulizi hayo yaliyoanza siku ya jumapili bado yanaendelea na kusababisha vifo na majeruhi wengi wakiwemo watoto.
Umoja wa mataifa umeelezea mashaka yake juu ya kutokea Allepo nyingine,ambapo ukombozi wa mji huo mwaka 2016 pia ulisababisha vifo vya mamia ya raia kufuatia mashambulizi ya vikosi vya serikali.
Mashambulizi yakiendelea katika mji es Ghouta Syria
''Makundi ya watoto ni miongoni mwa watu wanauawa huko Ghouta Mashariki.watoto hawa wanalipa gharama ya uhai wao kwa jambo ambalo hawahusiki.Kama tunahitaji kuzuia umwagikaji wa damu zaidi kwa watoto ni lazima tukubali kupata majeraha pia,na pia safari hii tunapata somo juu ya namna tunavyo takiwa kuwalinda watoto na kuona kwamba ni wajibu kila mmoja kuwalinda watoto.''
Idadi ya watu waliokufa ndani ya siku mbili ya mashambulizi hayo imepanda na kufikia 250 kwa mjibu wa ripoti kutoka Ghouta mashariki karibu na mji mkuu Damascus.





No comments:
Post a Comment