Waziri Kabudi azifunda mahakama nchini....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Salha Mohamed, Dar es salaam
SERIKALI imezitaka Mahakama kuendelea kutoka haki, kutochelewesha kesi bila sababu za msingi na kufungwa haraka masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha haki kutendeka.
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ameyasema hayo wakati akifunga maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyoambatana na kuzinduliwa kwa mahakama kadhaa ikiwemo mahakama ya wilaya ya Mkuranga, Bagamoyo, Kigamboni, Mahakama ya Mwanzo ya Kawe na kituo cha mafunzo kisutu.
Amesema mahakama inapaswa kutoa fidia ipasavyo, usuluhishi baina ya watu husika katika migogoro kwa wananchi kwa mujibu wa sheria.
Waziri huyo amezitaka Mahakama zipunguze kuchelewesha kesi bila sababu ya msingi ili mashauri hayo yaweze kukamilika kwa wakati.
Amesema anathamini mchango wa mahakama katika utoaji haki na kwamba ameridhishwa na maboresho yanayofanyika kila mwaka.
Profesa Kabudi amesema maboresho yanayoendelea katika mahakama nchini na namna ya kujipanga yanamstaajabisha kutokana na mahakama zilizozoeleka enzi hizo sasa zimebadilika.
"Naamini wizara na taasisi nyingine katika sekta ya sheria watajifunza kubadilika kama ambavyo hawakutegemea mahakama kubadilika," amesema
Ametoa rai kwa mahakama kuendelea na utaratibu wa matembezi kwakuwa yanajenga umoja na wadau.
Maonyesho hayo yaliongozwa na kauli mbiu 'Matumizi ya tehama katika utoaji haki na kuzingatia maadili'.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment