Zuma aomba kuongezewa miezi mitatu hadi sita..soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mashirika ya
Kimataifa
RAIS wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameomba kuongezewa muda wa kati ya miezi mitatu hadi sita ili ajiuzulu kwa hiari yake.
Rais Jacob Zuma
Hatua yake hiyo inafuatia kuwapo kwa shinikizo la ndani na nje ya chama chake cha ANC ambapo kimemtaka rasmi rais huyo ajiuzulu
baada ya kukataa kufanya hivyo mapema hii leo.
Hakujatolewa muda wa mwisho kwake kuondoka madarakani, lakini
imebainika kuwa mrithi wake atakuwa Cyril Ramaphosa ambaye ni rais wa
chama cha ANC.
Hatua hii ya ANC inaonekana ndio njia rahisi zaidi ya chama
hicho kumng'oa rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao
ungeweza kuwa mrefu na wenye madhara zaidi kwa chama cha ANC.
Rais Zuma ambaye anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa,
alishindwa uongozi wa chama tawala Desemba mwaka jana.
Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa anaongoza shinikizo za
kumuondoa Zuma katika nafasi yake hiyo ya Urais, na hatimaye kushika pia nafasi
hiyo.
Ramaphosa ameahidi pia kupambana na rushwa iliyokithiri na
kukijenga upya chama cha ANC, wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi
mwakani.
Iwapo Bwana Zuma, mwenye umri wa miaka 75, hatotekeleka,
atakabiliwana kura ya kutokuwa na imani naye bungeni ambayo anatarajiwa
kushindwa.
Akiwa amehudumu madarakani tangu 2009, ameandamwa kwa tuhuma za
rushwa.
Chama cha ANC hakijathibitisha rasmi mipango yake lakini duru
kutoka cham hicho zimetoa ufafanuzi katika vyombo vya habari nchini Afrika
kusini na pia kwa shirika la habara la kimataifa la Reuters.
Rais Zuma amekiuka shinikizo linaloongezeka la kumtaka ajiuzulu
tangu Desemba wakati Cyril Ramaphosa alipoichukua nafasi yake kama kiongozi wa
chama cha ANC.
Katibu mkuu wa ANC, Ace Magashule ameiwasilisha barua kwa
kiongozi huyo anayepigwa vita nyumbani kwake katika mji mkuu Pretoria, na
kumuarifu rasmi kuhusu uamuzi wa chama hicho wa kumtaka aondoke katika mkutano
na kamati ya kitaifa ya utendaji (NEC), taarifa zinasema.
No comments:
Post a Comment