Makonda azinyooshea kidole kampuni za udalali....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa onyo kwa kampuni za udalali zinazofanya kazi ya kukamata Pikipiki(bodaboda) kwa mtindo wa kuvamia kuacha mara moja kwa kuwa kitendo hicho kinahatarisha  usalama wa dereva na abiria.


Pia amezitaka kampuni hizo kuwasilisha nakala za nyaraka ya usajili kwa mwanasheria wa mkoa kuhakikiwa ili wapewe ushirikiano na serikali


Baadhi wa watendaji wa kampuni za udalali za jijini Dar es salaam wakiwa katika kikao na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam leo.


Ametoa maagizo hayo leo wakati alipokutana na Madalali wanaotekeleza hukumu za Mahakama na Bank kilicholenga kuwatambua na kupitia nyaraka zinazowapa mamlaka ya kufanya kazi hiyo ili wasionekane matapeli na waweze kupata ushirikiano wa serikali. 

Uamuzi wa Makonda kukutana na madalali unafuatia baada ya kusikia manyanyaso na ukandamizaji unaofanywa na baadhi ya madalali wanaopiga minada Nyumba, Magari, Viwanja, Mashamba, Ofisi na Mali za watu bila kufuata taratibu na kusababisha maumivu kwa wananchi. 

Amesema zipo kampuni za udalali zinazofoji nakala za hukumu, mihuri, sahihi za mahakama,ofisi ya Mkoa, Wilaya na Mitaa na wakati mwingine kufanya minada bila kufuata taratibu. 

Kutokana na hilo Makonda amezitaka kampuni zote za udalali Dar es salaam kuwasilisha nakala za nyaraka ya usajili kwa mwanasheria wa mkoa zipitiwe na kujiridhisha ili wapewe ushirikiano na Serikali.

Kwa upande wao Madalali wamemshukuru Makonda kwa uamuzi wa kuwatambua ili wapate ushirikiano wa Serikali kwakuwa wapo baadhi ya madalali waliokuwa wakifanya kazi hiyo kinyume na sheria na kuwachafulia kazi wale wenaofata taratibu za kazi hiyo. 

Akizungumzia bodaboda zinazokamatwa, Makonda amesema zipo baadhi ya kampuni zimekuwa zikivizia madereva wa bodaboda  kuwakamata na  kuwapiga kitendo ambacho amesema hawezi kukiruhusu kuendelea.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search