Ahukumiwa miaka minne jela kwa kumpa ujauzito binti yake...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Tabora

SADICK Masunzu (47) mkazi wa manispaa ya Tabora, amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi  Mkoa wa Tabora baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 16 na kumpatia ujauzito.


Akitoa hukumu hiyo jana, hakimu wa mahakama hiyo, Joctan Rushela alisema ameridhika na maelezo yaliyotolewa na upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili Tito Mwakalinga kuthibitisha bila shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Hakimu huyo aliongeza kuwa kitendo kilichofanywa na mshtakiwa si cha kiungwana katika jamii ya Watanzania, hivyo mahakama inamtia hatiani kwa kosa hilo na inamhukumu kwenda jela miaka minne ili liwe funzo kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Awali wakili wa Serikali, Mwakalinga alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alimbaka mtoto wake wa kumzaa na kumsababishia ujauzito.

Mwakalinga alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo katika tarehe tofauti Januari 2017 na kumsababishia ujauzito binti huyo aliyekuwa mwanafunzi wa Sekondari ya Lwanzali iliyopo katika Manispaa ya Tabora ashindwe kuendelea na masomo.

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kwa kuwa kitendo cha kumbaka na kumtia mimba mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi kimemharibia maisha yake.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search