Apandishwa kortini akituhumiwa kusafirisha gramu 214 za heroine...soma habari kamili na matukio360....#share
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu, imempandisha kizimbani Mfanyabiashara, Hariri Mohammed
Hariri (45), mkazi wa Kinondoni jijini
Dar es Salaam, kujibu Tuhuma za kusafirisha zaidi ya gramu 214 za dawa za
kulevya.
Mfanyabiashara, Hariri Mohammed Hariri (45) akiwa ameambatana na askari polisi katika viunga vya mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam.
Akisoma
hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Clara Chalwe mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu
Huruma Shaidi inadaiwa Machi 2 mwaka huu huko Kinondoni Matitu ndani ya Wilaya
ya Kinondoni mshtakiwa alisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride
zenye uzito wa gramu 214.11.
Hata
hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani kwa kuwa
Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevy isipokuwa
kwa kibali kutoka kwa DPP.
Kwa
mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Na
imeahirishwa hadi Aprili 4 mwaka huu
No comments:
Post a Comment