Waziri Mwakyembe amuonya Diamond.... soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu, Dar es salaam

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amemtaka msanii wa muziki Nassib Abdul ' Diamond Platinum' aache kulumbana na serikali




Dk Harrison Mwakyembe

Anaandika Mwakyembe;

Begin forwarded message:

From: Harrison George Mwakyembe <mwakyembe.harrison@gmail.com>
Date: March 20, 2018 at 6:31:41 PM GMT+3
To: solomonmwansele@gmail.com
Subject: Diamond

Nimesikitishwa sana na matamshi ya mwanamziki Diamond wakati akihojiwa na mtangazaji wa Times FM, Lil Ommy, kwa hatua ambazo Wizara inachukua kulinda maadili ya Kitanzania katika tasnia ya sanaa.

Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo na wasanii wawili kwa kukiuka maadili, yalifanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa Mhe. Naibu Waziri anayemlaumu. Diamond atambue kuwa Serikali ina taratibu zake. Maamuzi ya Naibu Waziri ni maamuzi ya Wizara.

Kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, however popular he is. Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake.

Si busara kwake kushindana na Serikali, na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya. Sijafurahishwa hata kidogo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search