Bavicha wapinga maamuzi ya waziri....soma habari kamili na matukio360...#share


Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

BARAZA la Vijana wa Chadema(Bavicha) limepinga hatua ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza kumfungia msanii Ibrahim Mussa “Roma Mkatoliki” kujihusisha na muziki kwa miezi sita.
Mwenyekiti wa barza la vijana Chadema (Bavicha) Patrich Ole Sosopi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Juzi Naibu waziri huyo alitangaza uamuzi huo dhidi ya msanii huyo kwa madai kuwa ameshindwa kufanya baadhi ya marekebisho aliyotakiwa kufanya kwenye wimbo wake wa “kibamia”

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi amesema naibu waziri huyo hana mamlaka hiyo bali wenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Baraza na Sanaa nchini (Basata).

“Tumesikitishwa sana kama baraza na kama chama, tunaona kwamba serikali hii inahamasisha watu wajiajiri, kama mtu amekosea na kama wimbo ni mbaya ni kwa nini wasiweze kusimamisha wimbo mmoja, tunaona kabisa kuna sura ya kisiasa na tunalaani kitendo hiki,” amesema Ole Sosopi.

“Roma Mkatoliki tumeona wakati mwingi akiendelea kuimba nyimbo za kiharakati na kiukombozi katika nchi hii na nyimbo zake nyingi zimekuwa zikionesha namna ya kukosoa serikali, naibu waziri hana mamlaka hayo ya kumfungia msanii bali ni Basata,” amesema Ole Sosopi.

Amesema Basata imeshindwa kufanya kazi yake kwa umakini na kuonesha kuwa linafanya kazi kwa maelekezo na kama wangekuwa makini na kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria walipaswa kufungia nyimbo mapema baada ya kutoka.

Ole Sosopi amesema kumfungia na kokaa bila kufanya kazi yake ni sawa na kitendo cha mauaji kwa sababu anasomesha, anategemewa na ndugu hivyo kumfungia kwa kipindi hicho maana yake asile, asisomeshe na kusimama katika maisha yake ya kawaida na kumfanya aidha awe kibaka ama mwizi.

Amesema kutokana na jambo hilo kama baraza litampa Roma msaada wa kisheria kwa kumpatia wakili atakayemsaidia kufungua shauri mahakamani ili kudai haki yake.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search