Gambo awaomba Lema, Calist kushirikiana na serikali...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Arusha


MKUU wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewaomba viongozi wa Chadema  jijini humo ambao ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema  na Meya wa Jiji la hilo, Calist Lazaro kushirikiana na serikali.
Godbless Lema                      Mrisho Gambo

Mrisho Gambo amesema hayo baada ya jana viongozi hao ambao anadai walikuwa wamealikwa kushiriki katika zoezi la utoaji wa mikopo kwa akina mama kutotokea kwa madai kuwa zoezi hilo lilikuwa likisimamiwa na serikali.

"Nipenda kutumia fursa hii kuwaomba viongozi wenzangu bila kujali itikadi ya vyama vyao maana leo tulimualika hapa mbunge, Meya na madiwani lakini wakasema tu sisi hatuendi sababu lile jambo linasimamiwa na serikali.

"Mimi nataka tu niwaombe viongozi wenzangu kwamba masuala ya maendeleo hayana vyama kwa sababu na sisi pia tungeangalia vyama pengine tungewaambia watu wa CCM wawape tu mikopo hiyo wanachama wao lakini tukasema sisi wenye serikali watu wetu ni wote bila kujali itikadi ya vyama vyao hivyo niwaombe wakubali kwamba Rais wa Tanzania ni Dkt. John Pombe Magufuli"

Aidha Mkuu huyo wa mkoa amezungumzia suala la maandamano ya April 26, 2018 kwa namna na kusema kuwa wapo watu wanafanya kazi ya kushawishi watu kuandamana lakini wao kama viongozi wanatoa njia za watu kupambana na maisha.

"Wakati wao wanahamasisha watu waandamane sisi tunawapa mbinu za kupambana na maisha, wakati wao wanahamasisha waandamane sisi tunawagea mitaji ili waweze kupata ridhiki na familia zao, wakati wao wanahamasisha waandamane Dkt John Pombe Magufuli anatoa elimu bure kwa shule zote nchi nzima" alisema Gambo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search